Taarifa za Jumla
Mradi wa Mikopo ya Uwekezaji na Msaada wa Utekelezaji (IFF – OBA) unazisaidia Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini (UWSSA) nchini Tanzania kugharimia uwekezaji mdogo wa miun-dombinu yenye kuleta matokeo ya haraka katika uzalishaji wa mapato kupitia mikopo ya kibiashara kutoka benki za ndani.
Kwa kushiriki katika programu ya Mikopo ya Uwekezaji na Misaada ya Utekelezaji, Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka Mijini nchini Tanzania zitagharimia uwekezaji wa miundombinu michache kwa kutumia mikopo ya kibiashara kutoka benki za ndani na zitapewa motisha hadi kiasi cha 50% ya gharama stahiki za uwekezaji baada ya kufikia mafanikio ya malengo ya utendaji yaliyowekwa awali.
Hatua muhimu zitakazochukuliwa na programu ya Mikopo ya Uwekezaji na Msaada wa Utekelezaji zimeelezwa katika Kielelezo hapa chini.
Vipeperushi vya IFF vinaweza kupakuliwa hapa.
Miongozo ya uendeshaji wa mradi wa IFF inaweza kupakuliwa hapa.