Mawanda ya Programu
Katika kipindi cha mkataba (Aprili 2016 – Septemba 2019) timu ya mradi wa Mikopo ya Uwekezaji na Misaada ya Utekelezaji itasaidia katika utekelezaji wa takribani miradi 35 ya uwekezaji wa miundombinu ya UWSSA ya karibu Euro milioni 20, inayohitaji takribani Euro milioni 10 za msaada ya uwekezaji.
Kwa hivyo, Mkopo wa Uwekezaji (IFF) utasaidia:
- Kutafuta vyanzo vya fedha vya ziada kwa ajili ya sekta ya Usambazaji wa Maji safi na Uondoshaji wa Maji taka Tanzania;
- Kuongeza ufanisi na mafanikioya rasilimali fedha chache zilizopo;
- Kuzidisha usimamizi mzuri wa maji kwa kuongeza nidhamu katika matumizi ya fedha, ufanisi, uwajibikaji, umiliki na wajibu wa Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka;
- Kuongeza ufanisi wa Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka;
- Kuongeza usambazaji wa maji kwa wakazi hivyo kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa nchi;
- Kuimarisha ujuzi, uelewa, na kuweka taratibu muhimu pamoja na miongozo ndani ya MoW, EWURA, Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka na benki zinazohusu masharti ya kutoa mikopo ya kibiashara.