Kustahili Kuomba Mkopo
Mashirika yanayotoa huduma za maji yaliyopo Tanzania tu ndiyo yanayostahili kuwasilisha maombi chini ya Mradi wa Mikopo ya Uwekezaji na Msaada wa Utekelezaji. Mashirika hayo yanawajibika kwa maombi yote ya mapendekezo ya miradi yakiwemo yale yaliyotolewa kwa niaba ya waendeshaji wadogowadogo katika maeneo yao ya kimamlaka.
Lazima ieleweke kwamba mkopo huu si mpango wa msaada bali unatolewa kwa kuzingatia Ma-tokeo ya Utekelezaji na masharti ya msingi ni kama yafuatayo:
- Mradi unaopendekezwa unapaswa kuwa unaongeza mapato au kupunguza gharama za uendeshaji.
- Mradi kiufundi unatekelezeka
- Mradi unaweza kuingiza faida, hii ina maana kuwa mapato yatakayozalishwa kutokana na mradi yanaweza kurejesha mkopo ndani ya kipindi cha mkataba wa mkopo (yaani mapato lazima yalipie malipo ya riba na mkopo);
- Mapato ya huduma yajumuishe gharama za uendeshaji;
- Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka iwe na kibali kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kupata mikopo ya kibiashara;
- Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka iwe na taarifa za ukaguzi wa fedha kwa miaka mitatu iliyopita;
- Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka iwe na mpango wa kibiashara uliopitishwa na EWURA pamoja na mradi huu ni sehemu ya mpango huo wa kibiashara;
- Upekee wa uwezeshaji mradi kifedha lazima uthibitishwe ili kuhakikisha kwamba mradi haufadhiliwi mara mbili.